Tuesday, August 9, 2011

MAADILI

kwanza nachukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema na fadhila kwa kunijahalia afya njema, baada ya hapo napenda kutoa  salamu zangu za dhati naomba niwashukuruni ndugu, jamaa na marafiki kkuweza kuzungumza,kudadavu mada kuu iliyopo hapo juu.
 Maadili ni kitu muhimu sana katika taifa letu la Tanzania na ulimwengu kwa ujumla wake,maana kama jamii inakumbwa na mmomonyoko wa maadili ndani ya jamii inapelekea kuzalisha taifa la watu wenye utapi mlo wa mawazo haswa rushwa,ubinafsi,uloho na uzandiki ndani ya nchi.
 jamii bora mara zote ujengwa kwa kuwepo na watu wenye maadili  safi,endapo jamii inakosa maadili hivyo inapelekea kuzalisha nchi maskini kwani mwisho wa siku tunakujapata viongozi wenye utapiamlo wa mawazo finyu juu ya anasa ya maisha yao tu. 

MADAWA YA KULEVYA

jamii inaendelea kutafunwa na janga zito ambalo kila kukicha linasababisha dhahama kubwa kwa maendeleo yetu kuanzia ngazi ya familia na hata taifa kwa ujumla. Ni nani wa kulaumiwa, hapana shaka hakuna mchawi wa hili ila ni jamii yetu husika ndiyo kikwazo kwa kulea uozo wa namna hii. Hakika MAADILI mema ndio msingi wa jamii endelevu! Maadili mema huanzia ngazi ya familia, kwa maana hiyo hata mmomonyoko wa maadili huanzia katika ngazi ya familia! Lengo la kuipa mzigo familia